Robo Mwezi. Massimo Longo E Maria Grazia Gullo

Читать онлайн книгу.

Robo Mwezi - Massimo Longo E Maria Grazia Gullo


Скачать книгу

       Robo Mwezi

       Watumishi wa Campoverde

       Imetafsiriwa na Kennedy Langat

       Hakimiliki © 2019 M.G. Gullo – M. Longo

       Picha ya jalada na michoro iliundwa na kuahiririwa na Massimo Longo

       Haki zote zimehifadhiwa

       ISBN

       ISBN-13:

       JEDWALI YA YALIYOMO

Sura ya Kwanza Anaepuka nikijaribu kumkumbatia...Sura ya Kwanza Anaepuka nikijaribu kumkumbatia...
Sura ya Pili Mnong'ono wa baridi ulikuwa ukimsumbuaSura ya Pili Mnong'ono wa baridi ulikuwa ukimsumbua
Sura ya Tatu Aligundua kuwa mvulana huyo alikuwa ametishika, na akaangua kicheko Sura ya Tatu Aligundua kuwa mvulana huyo alikuwa ametishika, na akaangua kicheko Sura ya Tatu Aligundua kuwa mvulana huyo alikuwa ametishika, na akaangua kicheko
Sura ya nne Sauti ilikuwa ikinong'oneza masikioni mwake maneno kwa lugha isiyojulikanaSura ya nne Sauti ilikuwa ikinong'oneza masikioni mwake maneno kwa lugha isiyojulikana
Sura ya Tano Anakabiliwa na kitu cha kuogofyaSura ya Tano Anakabiliwa na kitu cha kuogofya
Sura ya Sita Hakuweza kutoa matamshi hayo kutoka kwa kichwa chakeSura ya Sita Hakuweza kutoa matamshi hayo kutoka kwa kichwa chake
Sura ya Saba Wahusika wasioeleweka waliwashwa na sauti ya kutuliza Sura ya Saba Wahusika wasioeleweka waliwashwa na sauti ya kutuliza Sura ya Saba Wahusika wasioeleweka waliwashwa na sauti ya kutuliza
Sura ya Nane Tafakari ya picha hiyo mbayaSura ya Nane Tafakari ya picha hiyo mbaya
Sura ya Tisa Ngazi isiyo na mwishoSura ya Tisa Ngazi isiyo na mwisho
Sura ya Kumi Alihisi kama angeweza kutoboa mbingu kwa mikono yake waziSura ya Kumi Alihisi kama angeweza kutoboa mbingu kwa mikono yake wazi
Sura ya Kumi na Moja Wazo hili liliendelea kuitesa royo yakeSura ya Kumi na Moja Wazo hili liliendelea kuitesa royo yake
Sura ya Kumi na Mbili Ilimkumbusha kinywaji cha vitunguu vya kiberiti Sura ya Kumi na Mbili Ilimkumbusha kinywaji cha vitunguu vya kiberiti
Sura ya Kumi na Tatu Alishuka kutoka angani akikokota mawingu yake meusiSura ya Kumi na Tatu Alishuka kutoka angani akikokota mawingu yake meusi
Sura ya Kumi na Nne Alishuka chini ya winguSura ya Kumi na Nne Alishuka chini ya wingu
Sura ya Kumi na Tano Kama kwamba alimezwa na DuniaSura ya Kumi na Tano Kama kwamba alimezwa na Dunia
Sura ya Kumi na Sita Ghafula kelele za ajabu zilisikika kama za kigugumizi cha kinaSura ya Kumi na Sita Ghafula kelele za ajabu zilisikika kama za kigugumizi cha kina
Sura ya Kumi na Saba Alikuwa akitembea vizuri wakati alipovuka kizingitiSura ya Kumi na Saba Alikuwa akitembea vizuri wakati alipovuka kizingiti
Sura ya Kumi na Nane Makucha yaliingia ndani ya ngozi yakeSura ya Kumi na Nane Makucha yaliingia ndani ya ngozi yake
Sura ya Kumi na Tisa Kama kana kwamba ilikuwa Sukari ya barafu kupamba keki ya sifongo ya VictoriaSura ya Kumi na Tisa Kama kana kwamba ilikuwa Sukari ya barafu kupamba keki ya sifongo ya Victoria
Sura ya Ishirini Kila wakati mtoto akiniita kwa jina fulani, ndivyo nitakavyoitwaSura ya Ishirini Kila wakati mtoto akiniita kwa jina fulani, ndivyo nitakavyoitwa

       Dibaji

      "Kila kitu kitakuwa sawa, wewe ni mvulana mkubwa sasa....Rudi na ucheze na Watoto wengine. Tutakutana tena, ninakuahidi''

      Mtoto alimtazama akitiririkwa na machozi alipoondoka mtu ambaye amekuwa akicheza naye tangu mwanzoni.

      Mtoto alikimbia kurejea kwenye vijigari kwenye bustani iliyojuani, ambako alikwenda kucheza na watoto wengine jirani, huku fikra za rafiki ya kimawazo zikififia polepole.

      Baada ya kujipenyeza kwenye mahali watoto wengine walikuwa, hatimaye angeweza kupanda kwa kitelezo. Hakupoteza hata muda na alianza kuteleza kwenda chini ya kitelezo, akisukuma kwa bidii kadri awezavyo. Hakuteleza hata hadi mwisho, wakati alipoona msichana mwenye nywele nyeupe akikimbia kutoka kwa mama yake na kuelekea kwenye miguu yake. Hakuweza kupunguza mwendo na alimgonga kwa nguvu.

      Msichana huyo mdogo alipoteza mwelekeo na kugonga kichwa chake kwenye ukingo wa kitelezo.

      Alijaribu kumfikia mtoto huyo msichana ili kuhakikisha kuwa alikuwa sawa, lakini akasukumwa kando bila huruma na mamaye, ambaye alikuja kumwokoa. Ghafula, kundi la babu na akina mama walikusanyika karibu na msichana huyo maskini.

      Alipokuwa akijaribu kutambaa mbali na miguu ya watu wazima, alihisi kwamba alikuwa amezimia. “Mtu mmoja aliita ambulensi!” Huku sauti hiyo ikijitokeza kwa nguvu kwenye maskio yake, alianza kuingiwa na hofu. Alikimbia kuelekea msituni nyuma ya bustani.

      Ghafula, kila kitu karibu naye kikawa giza. Upepo baridi ulikuwa umesheheni sauti za kutisha. Mistari asiyoijua ilianza kuchanganyika na mazungumzo ya wazazi kwenye bustani. Zilikuwa zikitoka nyuma ya kundi la miti, ambayo vivuli vyao virefu vilikuwa vinajidhihirisha. Kisha, sauti hiyo ambayo ilikuwa ikijitokeza kutoka pande tofauti ilizidi kuendelea kusikika. Alikuwa akimfikia zaidi na zaidi, hadi alipohisi kuwa ilikuwa ikinong'oneza maskioni mwake:


Скачать книгу